Wednesday, October 21, 2009

Mambo yangu mapya!!!!


Nimefanya modeling fastafasta ya kichwa cha mtu katika kutangazia marafiki zangu kwamba sasa nimefungua ukurasa mpya katika medani ya filamu na teknolojia ya animation! Niko katika project yangu ya kwanza inayoitwa MZEE NA FIMBO ZAKE ni hadithi ya jadi.

Saturday, September 26, 2009

NAFICHUA SIRI SASA....

Walioiona filamu ya Sanda Nyeusi, walishangaa tu kwamba picha iliyofungua filamu ya makaburi ilipigwaje, ukweli ni kwamba japo inaonekana kuwa ni sawa na mazingira ya ukweli, lakini ni kazi ya 3D animation.

MIMI NA DIGITAL MEDIA

Mbali na kuwa ni mwandishi, mtengeneza filamu, pia sasa mimi ni Animator. Nimesoma mambo ya Digital Media ambayo yananiwezesha kutengeneza filamu za katuni na hata filamu za uhalisia, mfano ni baadhi ya matukio yaliyomo kwenye filamu ya Sanda Nyeusi ni mafanikio yaliyotokana na mafunzo hayo. Kazi hii ilifanywa na Chuo ninachosoma cha Media One Productions na mimi nikiwa miongoni mwa watendaji.
Kijumba unachokiona na mazingira yote nilikitengeneza kwa 3D, sio kijumba halisi.


"SANDA NYEUSI" KATIKA MAFANIKIO

KAZI NZURI
Filamu ya Sanda Nyeusi iliyotokana na kitabu nilichoandika na kukichapisha Novemba mwaka jana, imefanikiwa kuingia mitaani na kupata mauzo mazuri. Watu wengi wamenipigia simu na kunipongeza kwa kazi ile, wakisema ni nzuri na inaeleweka. Kwa niaba ya wenzangu wote tulioshiriki kutengeneza filamu hiyo, nawashukuru wote kwa kutupa moyo.
Filamu hii tuliirekodi mjini Morogoro na niliihariri mimi mwenyewe ikiwa ni kazi yangu ya kwanza tangu nilipomaliza mafunzo ya Digital Media yaliyohusisha 3D Animation na Motion Graohics.
PICHANI: Tukio mojawapo la filamu hiyo

Text Widget

Mahali pangu

Text Widget