KAZI NZURIFilamu ya Sanda Nyeusi iliyotokana na kitabu nilichoandika na kukichapisha Novemba mwaka jana, imefanikiwa kuingia mitaani na kupata mauzo mazuri. Watu wengi wamenipigia simu na kunipongeza kwa kazi ile, wakisema ni nzuri na inaeleweka. Kwa niaba ya wenzangu wote tulioshiriki kutengeneza filamu hiyo, nawashukuru wote kwa kutupa moyo.
Filamu hii tuliirekodi mjini Morogoro na niliihariri mimi mwenyewe ikiwa ni kazi yangu ya kwanza tangu nilipomaliza mafunzo ya
Digital Media yaliyohusisha
3D Animation na
Motion Graohics.PICHANI: Tukio mojawapo la filamu hiyo